Mkuu wa mkoa wa Kigoma Mhe. CP. Thobias Andengenye AMEPONGEZA uongozi wa Wilaya ya Buhigwe ukiongozwa na Mhe. Michael Ngayalina, Mkuu wa wilaya hiyo akishirikiana na timu ya menejimenti chini ya Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Essau Ngoloka, pamoja na kamati na uongozi wa shule zote za Sekondari kwa maendeleo mazuri ya ukamilishaji wa jumla ya vyumba 53 vyenye thamani ya Tsh 1,060,000,000 fedha zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Jemedari Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19. Pongezi hizo alizotoa wakati wa kukagua ujenzi wa miradi hiyo ya madarasa leo Desemba 30, 2021
"Mimi kwa niaba ya Timu ya mkoa niseme TUMERIDHISHWA na ukamilishaji wa ujenzi Buhigwe"
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz