Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndg. George Mbilinyi, leo Julai 5, 2024 ametembelea Ofisi mbali mbali za za serikali Wilayani Buhigwe kwa lengo la kufahamiana na kujenga umoja na mshikamano kati ya Halmashauri na Taasisi hizo katika kutekeleza majukumu kufikia Lengo la Mhe. Rais la kuwafikia wananchi kwa Huduma Bora.
Miongoni mwa Taasisi alizotembelea ni Pamoja na Mahakama ya Wilaya, TAKUKURU, Jeshi la Polisi na TARURA ambapo pia alisikiliza changamoto na ushauri kutoka kwa Taasisi hizo juu ya Halmashauri anayoiongeza ili kufanya maboresho na mabadiliko katika kutekeleza majukumu yake.
Akizungumza akiwa Jeshi la Polisi amewaomba kuongeza ushirikiano kwenye ukusanyaji wa mapato pale wanapohitajika, jambo ambalo ameliona ni muhimu kwa taasisi hiyo kuwa kitu kimoja katika kufikia au kuvuka malengo ya Bajeti katika kukusanya mapato.
Mbilinyi pia amezitaka taasisi hizo kujenga Utamaduni wa kuandaa na kufanya matukio ‘events’ kwa lengo la kuendelea kujenga ukaribu, upendo, umoja na mshikamano miongoni mwa watumishi wa taasisi za serikali wilayani hapo.
Mkurugenzi Mbilinyi amekuwa muumini wa Ushirikiano baina ya watumishi na taasisi pasipo kujali tofauti ya ofisi na majukumu ili kutekeleza Majukumu kikamilifu na kufikia Malengo na nia ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassana, Rais wa JMT kuwaletea wananchi wa Buhigwe maendeleo.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz