Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndg. George Emmanuel Mbilinyi atembelea na kukagua mradi wa umaliziaji wa shule mpya ya Sekondari ya wasichana Kahimba iliyopo kata ya Kajana kijiji cha Kasumo
Mradi huu ulipokea kiasi cha Shilingi Million mia tisa na sitini (960,000,000) tarehe 08.10.2024 toka Serikali Kuu kupitia Mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).
Hata hivyo mradi umepokea vifaa vyenye thamani ya Tsh milioni 100 kutoka Bank ya NMB na kufanya shule kupokea jumla ya Tsh. Billion 1 na million 60
Mradi huu umelenga kukamilisha Mabweni mawili nyumba moja ya mwalimu (2in 1), nyumba ya kulala wagonjwa (sickbay), maabara ya kemia na biolojia, vyumba 12 vya madarasa, matundu 22 ya vyoo na jengo la utawala. Shule ya sekondari Kahimba itafunguliwa Januari 2025 na tayari imekwishapangiwa wanafunzi 80 wa kidato cha kwanza.
Shukrani za pekee ziende kwa Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa maono haya ya kujenga shule za wasichana nchini na kutufikia Buhigwe.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz