Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina amemtaka Mwenyekiti Msaidizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mh Diwani Robson Mzimya kurudisha imani kwa wanabuhigwe.
Ameyasema hayo alipohudhuria baraza la madiwani kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika kata za Buhigwe pamoja na Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti na Kuundwa kwa kamati za kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.
“Ninapenda kukupongeza kwa kupata kura zote za ndio,ni heshima kubwa lakini ni imani ambayo Waheshimiwa wameweka juu yako,Mh Rais huwa anapenda kusema ukipewa imani rudisha imani,na mimi kwenye hilo la kurudisha imani napenda kukwambia neno moja itendee haki imani ambayo wameweka juu yako”.alisema Kanali Ngayalina
Sambamba na hilo aliwaasa waheshimiwa madiwani,viongozi na wote waliohudhuria kushirikiana kwa pamoja katika kutoa elimu na kuhamasisha Wananchi kujitokeza kujiandikisha na kupiga kura tarehe 27 mwezi Novemba 2024.
Naye Mwenyekiti Msaidizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mh diwani Robson Mzimya alisema kuwa yupo tayari kufanya kazi kwa kushirikiana na uongozi uliopita kwa ajili ya kujenga nyumba moja ya taifa la Tanzania
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz