Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina ameyataka Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali kuzingatia kanuni na sheria wakati wa utendaji kazi wao. Ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika kikao cha kuwasilisha taarifa za robo ya utekelezaji kazi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwa Julai-Septemba na Oktoba 2024.
Aidha amesisitiza kuwa Kuna sheria nyingi zinazohusu utendaji kazi wa mashirika hayo hivyo kuwataka kupitia sheria hizo mara kwa mara na kuhakikisha wanazitekeleza kadri walivyoelekezwa.
Sambamba na hilo ameongezea kwa kuwaasa kulinda maslahi ya Watanzania ikiwemo kulinda mila na desturi za nchi pamoja kuwafikia walengwa wa miradi yao na kushiriki kikamilifu katika vikao wanapohitajika.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz