Mkuu wa mkoa wa Kigoma IGP (mst) Balozi Simon Sirro katika maadhimisho ya sikukuu ya Nanenane amewataka wakulima kutumia fursa za mafunzo wanayoyapata wakati wa maonesho ya Nanenane kuwanufaisha kupata mazao yenye tija.
Haya ameyasema Mh. Balozi Sirro wakati kwa kuhitimisha maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ipuli Mkoani Tabora Leo tarehe 8 Agosti, 2025 yaliyojumuisha wadau mbalimbali.
"Ili kuweza kupata masoko nje na ndani ya nchi lazima kuwe na vifungashio vinavyoonesha viungo vilivyopo katika bidhaa kwa lengo la kujitangaza zaidi, hivyo maonesho haya yatumike kuwakutanisha wakulima wakubwa na wadogo kupata fursa za kukutana na masoko makubwa" alisema Balozi Sirro
Vilevile Balozi Sirro ameongezea kwa kuwasihi wafugaji kushiriki kikamilifu katika Zoezi la uchanjaji ili kuzuia vifo vitokanavyo na magonjwa ya mifugo
Kwa niaba ya wakuu wa Wilaya mkoa wa Kigoma Mh. Mwakisu ameishukuru Serikali ya Awamu ya sita ya Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa Kilimo kwa kutoa mbolea ya ruzuku kwa ajili ya Kilimo chenye tija na kuongeza mnyororo wa thamani katika mazao.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz