Tarehe 13 Julai 2024 Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata katika jimbo la uchaguzi la buhigwe walipata Mafunzo ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotarajiwa kuanza Julai 20, 2024. Pamoja na mafunzo ya ujazaji wa fomu zitakazotumika wakati wa uboreshaji wa taarifa za wapiga kura Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata walifundishwa matumizi ya mfumo wa kompyuta wa uandikishaji wapiga kura ujulikanao kama ( bayometric voters registration).
sambamba na zoezi la mafunzo ya Afisa Uandikishaji Jimbo la Buhigwe Ndg. Hamza Seif Mnaliwa aliwaapisha mawakala wa vyama vya siasa na kuwapatia elimu juu ya umuhimu na wajibu wa mawakala kuelekea zoezi la uboreshaji daftari lakudumu la wapiga kura.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz