Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe wanapatiwa mafunzo elekezi kwa siku mbili kuhusu maswala mbalimbali ya kiutendaji ikiwemo Historia na uhalali wa Serikali za Mitaa, Usimamizi wa Fedha za Miradi n.k.
Akizungumza na Waheshimiwa Madiwani waliohudhuria mafunzo hayo, katika hotuba yake ya ufunguzi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Buhigwe, Ndg. Peter Masindi ambaye pia ni mwakilishi wa Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, amewaasa kuwa na maadili mema ya uongozi, uwajibikaji, utawala bora na kuibua vyanzo vipya vya mapato.
Baada ya neno la ufunguzi kutoka kwa Mgeni rasmi, Wawezeshaji kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Dodoma, CPA CHARLES K. MATEKELE na ADV. PETRO NZIKU wakawaongoza wajumbe kupata M/kiti wa Mafunzo, ambapo Mhe. Eles Gomwa alipigiwa kura na kushika wadhifa huo.
Kisha wajumbe waliweka kanuni za mafunzo ikiwemo kuweka simu kwenye mitetemo, kuheshimu mawazo ya kila mjumbe, kunyoosha mkono endapo kuna swali au hoja, kutokutoka nje bila idhini ya Mwenyekiti.
Mwisho wawawezeshaji walianza kutoka mafunzo kwa kuanza na mada ya kwanza inayosema "Historia na Uhalali wa Serikali za Mitaa".
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz