Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe Ndg George Emanuel Mbilinyi Leo Juni 10,2024 amepokea ugeni wa Madaktar Bingwa wa Mama Samia ofisini kwake.
Madaktar hao wamekuja kwa lengo la kutoa huduma za matibabu mbali mbali kwa wananchi wa Wilaya ya Buhigwe na watakuwepo kwa muda wa siku tano wakitoa huduma hiyo katika hospital ya wilaya ya Buhigwe.
Wananchi wote mnakaribishwa kupata huduma mbali mbali za Magonjwa yasiyoambukizwa mjulishe na mwenzio ili asije akajilaumu kutokupata taarifa ya ujio wa madaktar hawa katika Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe Huduma Bora Fahari Yetu.
Magonjwa yatakayopatiwa ufumbuzi au matibabu na Madaktar Bingwa wa Mama Samia nikama ifuatavyo Huduma ya Afya ya watoto wachanga
Huduma ya Afya ya Uzazi,wajawazito na Magonjwa ya Wanawake
Huduma ya Magonjwa ya Shinikizo la Damu
Huduma ya upasuaji
Huduma za Ganzi na usingizi
Huduma ya Tiba ya Magonjwa ya Dharura na ajali.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz