Maandalizi ya mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2026 yameanza rasmi katika Wilaya ya Buhigwe kwa kuanza kufanya tathmini ya mbio hizo kwa mwaka 2025.

Katika kikao cha maandalizi kilichoongozwa na mwenyekiti Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina amewapongeza wajumbe wa kikao hicho kwa juhudi zilizowezesha Wilaya hiyo kushika nafasi ya nne kimkoa kwa mwaka 2025 kutoka nafasi ya nane kimkoa kwa mwaka 2024.

Aidha amewaasa wahusika wote kujiandaa mapema kwa kupitia miradi itakayopitiwa na mbio hizo za mwenge.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz