Katika kukabiliana na Utapia mlo kwa wilaya ya Buhigwe ambao hadi sasa ni zaidi ya Asilimia 40, kikao kazi cha wajumbe wa kamati ya Lishe kiwilaya imekaa kupanda bajeti ya Afua za lishe kwa mwaka wa Fedha 2022/2023
Akizingumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Buhigwe Ndg. Essau Ngoloka amesisitiza Bajeti inayopangwa kufikiwa na ameahidi ofisi yake kusimamia kukikamilifu kuona fedha zilizotengwa kutolewa kwa ajili ya kutekeleza Afua za lishe ili mipango ya kukabiliana na Utapia mlo kufikiwa na ikiwezekana kutokomeza Utapia mlo wilayani hapo.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz