Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ndugu George E Mbilinyi amewakabidhi vitendea kazi maafisa ugani wa Wilaya ya Buhigwe.
Aliwakabidhi vifaa hivyo katika kikao alichokaa na maafisa ugani wote wa Wilaya katika ukumbi wa Halmashauri hiyo ikiwemo nguo maalum za maafisa ugani na pikipiki mbili.
Aidha aliwaasa kuzingatia yale yote waliyoelekezwa na Mh Rais Samia Suluhu Hassani ikiwemo kukaa katika vituo vyao kazi kwa ajili ya kuwasikiliza na kutatua changamoto za Wakulima na Wafugaji katika kikao na maafisa ugani kilichofanyika Agosti mwaka huu Ikulu Dodoma.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz