Buhigwe, Kigoma: Septemba 11, 2023
Mhe. Col. Michael Masala Ngayalina, Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe leo Septemba 11, 2023 ameyasema hayo wakati wa Kikao kazi cha Wajumbe wa Kamati ya Afya Msingi cha kupanga Mikakati ya kuwafikia Watoto 105,000 wenye umri chini ya Miaka Nane kwa ajili ya Chanjo ya POLIO inayotarajiwa kuanza ALHAMISI ya Tarehe 21.09.2023 hadi JUMAPILI ya Septemba 24, 2023
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa kikao kazi hicho Mhe. Ngayalina amesisitiza wajumbe hao kutoa elimu juu ya Chanjo hiyo na kusisitiza kutumia majukwaa na nafasi zao kuondoa uvumi wowote wenye nia ovu ya kukwamisha zoezi
Ameongeza kuwa kuna umuhimu wa Jamii kuambiwa ukweli juu ya madhara yatokanyo na Ugonjwa huo na kuwekwa wazi kuwa HAUTIBIKI bali kujaribu kukabiliana na adhari zake baada ya mtu kupatwa na Ugonjwa huo unaoshambulia hasa mishipa ya Fahamu
“Hakuna mtoto, kaya, kitingoji, Kijiji wala kata itakayoachwa kufikiwa kwenye zoezi hili la Chanjo kwa wilaya ya Buhigwe, mimi mwenyewe ninazunguka sana kupitia na kuona changamoto na kuzitatua kwa wakati ili kufikia malengo” alisisitiza DC Ngayalina
Baadae Mganga mkuu wa Wilaya hiyo DKT. Innocent Mhagama aliendelea kutoa uelewa na kujadili mikakati kabambe iliyowekwa ili kufikia Watoto wote walengwa ambao ni wenye umri chini ya miaka Nane.
“Ugonjwa wa POLIO huambukizwa na Virusi vya Polio na hauna tiba na unaweza kusababisha kupooza kwa ghafla, kubaki na ulemavu wa kudumu au kifo
Dalili za ugonjwa POLIO ni Pamoja na Ulemavu wa ghafla wa viungo, Homa, Mafua na maumivu ya mwili, kichwa na shingo na kuongeza kuwa watu walio hatarini Zaidi ni Watoto chini ya miaka 15 ingawa unaweza kuwapata watu wa rika zote
Athari za Uginjwa wa Polio ni ulemavu wa kudumu wa miguu, mikono au kifo
Kumbuka: “Kila tone la chanjo ya polio, humkinga mtoto dhidi ya ulemavu na kifo, Mpeleke Mtoto Apate chanjo”. Alimaliza DKT. Mhagama.
Utekelezaji wa zoezi la chanjo kwa wilaya ya Buhigwe linatekelezwa kwa Nyumba kwa Nyumba kwa tarehe 21-24.09.2023 kwa Watoto wenye Umri chini ya Mikaka 8 chini ya Kauli ya:-
“Mpe Matone………….Okoa Maisha”
Silas, J
Afisa Mawasiliano Serikalini
Buhigwe
Buhigwe
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz