Kikao cha baraza la Madiwani kilianza kwa kamati kukutana kwaajili ya kuvunja kamati hizo. Kwakuwa hiki ni kikao cha mwisho wa mwaka na kutokana na kanunu na sharia Kabla ya kuunda baraza jipya pamoja na kuteua Mwenyekiti Mwengine kwa mwaka wa fedha 2017/18 kamati hizo zinatakiwa zivunje ili kuteua kamati mpya pamoja na wenyeviti wake.
Kikao hiki kilikuwa na Agenda kuu zifuatazo.
Baada ya kuwasilishwa kwa Agenda tajwa hapo juu, Makamu mwenyekiti Mh. Diwani Luzibila kutoka kata Munzeze alifungua kikao kwa kusoma Dua ya kikao hicho kwa kikiombea amani na Busara iwaongeza katika kufanya maamuzi kwaajili ya Halmashauri.
Agenda ya pili iliwasilishwa na Afisa Mipango wa Wilaya Ndg. Charles Mduma, Taarifa hiyo ilipokelewa na kujadiliwa na Waheshimiwa Madiwani.
Agenda ya tatu ni kupitisha ratiba ya Vikao vya kisharia vya Halmashauri, Hoja ya Waheshimiwa Waliomba Menajimenti kuhakikisha ratiba hiyo inafuatwa kikamilifu na kama kuna dharura basi wapewe taarifa mapema ili nawao waweze kupanga ratiba nyengine.
Agenda ya Nne ilikuwa agenda ya kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Wake. Agenda hii ndio agenda ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kuona nani atachukua nafasi hizo mbili.
Waheshimiwa Madiwani Walimtaka Mkurugenzi awaongeze katika kanuni na taratibu zitakazo tumika katika kufanikisha uchaguzi huo pamoja na muundo wa kamati baada ya uchuguzi. Aidha mkurugenzi alimtaka Afisa utumishi afafanue kanuni na sharia ambazo zitawaongoza.
Majina ya Wagombea ni kama ifuatavyo:-
MWENYEKITI WA HALMASHAURI:-
Mh. VINANCE KIGWINYA:
Mh. MOSHI BUKEBUKE:
MAKAMU MWENYEKITI:-
Mh. HAMIS LUKANKA:
Mh. PASCAL NKEYEMBA:
Baadaya ya uchaguzi matokeo ya kura yalikuwa kama ifuatavyo:-
UPANDE WA MWENYEKITI:
JUMLA YA KURA: 27
KURA ILIYOHARIBIKA: 1
Mh. VINANCE KIGWINYA: Alipata kura 16
Mh. MOSHI BUKEBUKE: Alipata kura 10
UPANDE WA MAKAMU MWENYEKITI:
JUMLA YA KURA: 27
KURA ILIYOHARIBIKA: 1
Mh. HAMIS LUKANKA: Alipata kura 16
Mh. PASCAL NKEYEMBA: Alipata kura 10
Baada ya matakeo hayo Mwenyekiti alimtanga Mh. Venance Kigwinya ambaye ni Diwani wa kata ya Buhigwe (Kulia Mwa picha) kuwa ni Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri ya Wilaya Buhigwe.
Aidha kwa upande kwa Makamu Mwenyekiti, Mh. Hamis Lukanka (Kushoto mwa picha) ndio makamu mwenyekiti kwa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.
Baada ya Uchaguzi huu Waheshimiwa Waliteu Kamati Mbali mbali.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz