Kikao kilifunguliwa mnamo saa 10:24 asubuhi na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la wilaya Col Marco E. Gaguti na kukaribisha wajumbe wa baraza ambao ni Sekta Binafsi na Sekta ya Umma pamoja na wageni kutoka mkoani ambao ni meneja wa mradi LIC, Afisa Biashara wa Mkoa na Mratibu wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC).
Kikao kiliendelea kwa kuendeshwa na Sekretarieti ya wilaya ambapo wajumbe walijitambulisha mmoja mmoja na kumalizia na meza kuu ambapo ilikuwa na Mwenyekiti wa Baraza (DC), Katibu (DED), Mwenyekiti wa Halmashauri na Mwenyekiti wa TCIAA wilaya ya Buhigwe.
Kutoka kushoto mwa picha ni Mwenyekiti wa TCIAA wilaya ya Buhigwe(Ndg. Azalia A. Kolobo), Elihuruma J. Nyella (Katibu wa kikao) akifatiwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe (Col Marco E. Gaguti) ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la biashara wilaya ya Buhigwe, na mwisho ni Mwenyekiti wa Halmashauri (Mhe. Venance Kigwinya).
Sekretarieti iliendelea kwa kusoma na kuhakikisha Agenda zilizotakiwa kujadiliwa siku hiyo, wajumbe walizipitia na kuhakiki kisha Sekretarieti ilisoma muhtasari wa kikao kilichopita cha Baraza la Biashara cha tarehe 29/9/2017. Baada ya Sekretarieti kuongoza wajumbe wa Baraza katika kusoma muhtasari huo ndipo kipengere cha yatokanayo kilifuata huku Mwenyekiti akifuatilia kwa ukaribu maazimio na utekelezaji wake.
AGENDA:
Urasimishaji wa Biashara wilaya ya Buhigwe.
Agenda hii iliwasilishwa na Afisa Biashara wa Mkoa ambapo alielezea umuhimu wa urasimishaji wa biashara unafanya wafanyabiashara kuwa rasmi na kutambulika nchini katika biashara zao. Aliendelea kwa kuwasisitiza wafanyabiashara kujipatia TIN namba kwa kuwa ni bure kwa watu wote ili kurahisisha urasimishwaji huo wa Biashara. Wajumbe wa Sekta binafsi waliulizwa maswali kama tofauti kati ya TIN namba na kujisajili na majibu yote yalijibiwa na Afisa Biashara wa Mkoa.
Agenda hii ilifungwa na Mwenyekiti kwa kutoa azimio kwamba LIC na wadau wengine wasaidie ili elimu hii iwafikie wafanyabiashara wote.
Afisa Biashara wa Mkoa akieleza umuhimu wa urasimishaji wa biashara.
Mpango mkakati wa kufanya mnada wa Wilaya ya Buhigwe kuendelea kufanya kazi. Katika agenda hii Afisa mifugo alielezea kwa kina kwa wajumbe na kuelezea kuwa jitihada za kuzuia mifugo isivushwe nje ya nchi ni kubwa sana ingawa inakwamishwa kutokana na maafisa mifugo kuwa wachache wilaya nzima ya Buhigwe.
Zoezi la upigaji chapa wa mifugo.
Afisa mifugo alifafanua kuhusu zoezi hili kwa wajumbe na kuelezea umuhimu wa kufanya au kupiga chapa. Alitoa wito kwa wafugaji na wafanyabisahara wa mifugo kupeleka ng’ombe kwenye chapa kwa ajili ya usalama, utambulizi na uhalali wa mifugo hiyo. Agenda hii ilifungwa na Mwenyekiti kwa kutoa maazimio kwamba mnada uanze ifikapo tarehe 03.01.2018, kufanya doria ili kudhibiti mifugo kutoroshwa nchi za jirani, wafanyabiashara waainishiwe njia maalumu watakazozitumia kupitisha mifugo yao.
Afisa mifugo(W) Ndg. Kenneth Tefurukwa akieleza umuhimu wa zoezi la upigaji chapa mifugo.
Mpango mkakati wa kuboresha mnyororo wa thamani.
Afisa kilimo alifafanua zao la mchikichi na ndipo wajumbe wakaanza kuchangia mada na wakahoji kwamba kwa nini zao la kahawa halikuainishwa na kupewa kipaumbele. Ndipo mwenyekiti aliamuru kwamba mkakati kuhusu vipaumbele vya wilaya ya Buhigwe viainishwe.
Upatikanaji wa pembejeo za ruzuku.
Katika agenda hii ilionekana wakulima wanafata mbolea kwa wakala mkubwa wilaya ya Kasulu hivyo wajumbe wakaomba apatikane wakala katika wilaya yetu ya Buhigwe ili kuondoa usumbufu kwa wakulima. Agenda hii ilifungwa na mwenyekiti kwa kutoa azimio kwamba wananchi (wakulima) wajiorodheshe na kwenda kununua mbolea kwa wingi, na pia alitoa fursa kwa wafanyabiashara watakaoweza kuwa mawakala ili kutatua tatizo hili.
Ushirikishwaji wa sekta binafsi katika maamuzi yanayofikiwa na sekta ya umma.
Wajumbe wa sekta binafsi walihoji kwamba ushirikishwaji haupo kwasababu ya kuona matangazo kuhusu ununuzi wa viwanja na hawajawahi kushirikishwa. Katibu wa kikao alikiri kutokea kwa jambo hilo na kuwatoa hofu wajumbe kwamba mikataba iko tayari na zoezi hilo litaanza hivi karibuni. Mwenyekiti alifunga agenda hii kwa kusema kwamba mawasiliano baina ya sekta hizi mbili yaboreshwe.
Kikosi kazi kiwezeshwe ili kimalizie zoezi la ufatiliaji wa maazimio yanayofikiwa na vikao vya Baraza la Biashara.
Wajumbe walihoji kwamba kazi za ufatiliaji wa maazimio zimeshindwa kufanyika kwasababu kulikuwa hakuna uwezeshwaji kwa kikosi kazi hivyo iliamuliwa kikosi kazi hiki kisitolewe bali kimalizie kazi ili kilete mrejesho baraza la Biashara lijalo. Pia manager (LIC) aliahidi hadi tarehe 20/12/2017 itakuwa imewezesha kikosi kazi hiki.
Uanzishwaji, uendelezwaji na usajili wa viwanda vidogo na vya kati.
Agenda hii iliibuliwa kwa kuwa na umuhimu wa Tanzania ya Viwanda. Ni agizo la kitaifa kwamba kila mkoa uwe na viwanda visivyopungua 100. Mwenyekiti alishauri ili agizo hili liweze kutimia yapatikane maeneo yaliyopimwa ili iwe rahisi hata wawekezaji wakija iweze kuwa rahisi kwao.
Changamoto zinazokwamisha masoko ya mpakani kufanya kazi.
Agenda hii iliibua majadiliano ambapo ilionekana masoko ya mpakani yana changamoto za wanajeshi kuchukua ushuru kwa wafanyabiashara. Swala hili limekuwa kikwazo sana na kufanya baadhi ya wafanyabiashara hata wa nchi jirani kuogopa kufika kwenye masoko yetu hayo. Mwenyekiti alifunga agenda hii kwa kuwatoa hofu wajumbe na kwamba swala hili litafanyiwa kazi hivyo wafanyabiashara wafanye biashara kwa amani.
Baada ya agenda hizi kujadiliwa kulikuwa na taarifa kutoka Sekretarieti kuhusu ushuru wa huduma. Wafanyabiashara walielezwa kwamba wajiandae kwa maana elimu hii itawafikia. Ushuru wa huduma ni muhimu kwasababu huongeza mapato kwenye halmashauri na kwamba ipo kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa. Hivyo wafanyabiashara walisisitizwa kujiandaa na elimu hiyo itakayotolewa.
Baada ya taaifa hiyo kulikuwa na agenda za ziada ambazo zilielezewa na wageni kutoka mkoani kama Afisa biashara wa mkoa na afisa sera (LIC).
MENGINEYO:
Mwenyekiti wa Baraza la Biashara alimalizia kikao kwa kukaribisha wageni wa mkoani washukuru kwa dakika 2 kila mtu.
Mwenyekiti wa halimashauri alimalizia kwa kushukuru wajumbe wa Baraza na waalikwa na ndipo Mwenyekiti alifunga kikao cha Baraza la Biashara mnamo saa 16:45 jioni hadi kikao kingine mwezi wa 3.
MAAZIMIO:
Na.
|
Ajenda
|
Maazimio
|
1.
|
Urasimishaji wa biashara Wilaya ya Buhigwe.
|
|
2.
|
Mpango mkakati wa kuufanya mnada wilaya ya Buhigwe kuendelea kufanya kazi.
|
|
3.
|
Mpango mkakati wa kuboresha mnyororo wa thamani.
|
|
4.
|
Ushirikishwaji wa sekta binafsi katika maamuzi yanayofikiwa na sekta ya umma.
|
|
5.
|
Kikosi kazi kiwezeshwe ili kimalizie zoezi la ufuatiliaji wa maazimio yanayofikiwa katika vikao vya baraza la biashara.
|
|
6.
|
Upatikanaji wa pembejeo za ruzuku.
|
|
7.
|
Uanzishwaji, uendelezwaji na usajili wa viwanda vidogo na kati.
|
|
8.
|
Zoezi la upigaji chapa kwenye mifugo.
|
|
9.
|
Changamoto zinazokwamisha masoko ya mpakani kufanya kazi.
|
|
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz