Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mh Godfrey M,Kasekenya amemtaka Mkandarasi wa Mradi Ambata wa Shule ya Sekondari kwa kidato cha tano na sita ya Buhigwe kukamilisha mradi huo kwa wakati na kwa ubora wa viwango vinavyostahili.
Ameyazungumza hayo leo tarehe 10 mwezi 1,2025 katika ziara yake Wilayani hapa ya kukagua Mradi wa barabara inayotoka Buhigwe Manyovu kupitia Kasulu kwenda Kibondo wenye jumla ya umbali wa Kilomita 260.
Mradi huu wa barabara unagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 9.Ikihusisha miradi ambata ambayo ni,Mradi wa usambazaji wa maji Manyovu na Buhigwe Bilion 5,mradi wa Stendi ya magari na soko buhigwe wenye gharama ya Milioni 700,Shule ya Sekondari kwa kidato cha tano na Sita wenye gharama ya Bilioni 3.7 yote ikitakiwa kukabidhiwa mwezi wa sita mwaka huu wa 2025.
Aidha amewataka Wakandarasi Wazawa kuongeza umakini na kasi ya kazi zao ili kuongeza zaidi thamani yao katika miradi nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina amemshukuru Naibu Waziri Kasekenya kwa ujio huo na kuahidi kufuatilia kwa umakini ujenzi wa miradi hiyo ili kukamilika kwa wakati kama alivyoagiza.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz