Kamati Ulinzi na Usalama ya wilaya ya buhigwe imefanya ziara leo 03.01.2024 ya kukagua miradi ya boost inayotekelezwa katika kata za Bukuba, Janda Munzeze, Mwayaya, Muhinda, Kibwigwa na Buhigwe
Akizungumza katika ziara hiyo Mh.Mkuu wa Wilaya amesema kuwa kuna baadhi ya shule wamesimamia vizuri miradi yao na kukamilisha kwa asilimia zote na viwango vinavyotakiwa na kuna wengine ambao wameonesha uzembe katika kusimamia miradi yao na haijakamilika kwa kiwango kinachotakiwa huku fedha ikiwa imemalizika.
Aidha, kamati imemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhingwe kuchunguza na kuhakikisha anawachukulia hatua sitahiki wale wote walionyesha uzembe katika miradi yao ili kuwa mfano kwa wengine wenye miradi ya kusimamia kutoleta uzembe tena na kufanya kazi katika viwango vinavyotakiwa na kwa muda uliopangwa.
Hata hivyo, maelekezo ya serikali ni kuwa kila darasa linatakiwa kuwa na dawati 15 jamba ambalo wengine. Pamoja na hayo pia kuna miradi mingine imekamilishwa kwa asilimia zote kwa viwango vya juu ambayo iko tayari kutumika januari hii shule zitakapofunguliwa madawati meza madarasa miundombinu yote iko sawa na wanatamani shule zifunguliwe haraka ili wanafunzi waanze kutumia miundombinu hiyo.
Kamati hiyo imetoa maelekezo ya jumla katika ziara hiyo hususani kuwa makini katika kusimamia na kuzingatia matumizi mazuri ya rasilimali zinazoletwa kwaajili ya kuikuza elimu na kutimiza malengo ya serkali yetu pia waende na mpango wa matumizi kama unavyoletwa wasifanye kinyume kwa nia ya kujinufaisha na nafsi zao.
Wakati hayo yakiendelea mwalimu mmoja amepata zawadi kwa kusimamia vizuri ujenzi wa darasa la awali viti na meza za Watoto sehemu ya michoze ya Watoto maarufu kama bembea na nyumba ya mwalimu two in one kwa viwango vyote vinavyotakiwa.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz