KAMATI YA SIASA MKOA WA KIGOMA YATEMBELEA MIRADI BUHIGWE.
Posted on: February 28th, 2025
Kamati ya siasa mkoa wa Kigoma ikiongozwa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Christopher Palanju leo tarehe 27 mwezi wa pili mwaka 2024 imetembelea miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Christopher Palanju ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kwa kusimamia vizuri miradi na kuwaasa kuongeza nguvu zaidi ya kusimamia miradi hiyo ili kuzitendea haki fedha zinazoletwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina ameishukuru kamati ya siasa Mkoa kwa kutenga muda wao na kuja kuitembelea Wilaya ya Buhigwe na kuahidi kuendelea kulitumikia taifa kwa Weledi pamoja na kutoa huduma bora kwa Wananchi.
Kwa upande wao Wananchi wa Wilaya ya Buhigwe wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuwaletea miradi ya kimaendeleo ambayo imerahisisha maisha yao kwa ujumla.
Katika ziara hiyo wametembelea shule ya sekondari Kahimba ya wasichana,mradi wa maji ,ujenzi wa Barabara za lami zinazo zunguka mji wa Buhigwe,mradi wa vijana wanaojishughulisha na upasuaji wa mbao kwa mashine za kisasa zinazotokana na mkopo wa asilimia nne wa Halmashauru na zahanati ya nyamihanga.#buhigwefahariyetu #2025kaziiendelee