Hata hivyo kamati hiyo ilianza na ukaguzi wa miradi inayotekleza wilayani hapo na kisha kufuatiwa na kikao cha kupokea taarifa za utekelezaji za divisheni na vitengo kwa robo ya pili na kuzijadili.
Pamoja na hayo pia walipokea taarifa za miradi yote iliyokaguliwa na kuzitolea ufafanuzi na maelekezo ya kukamilishwa kwa muda uliopangwa kwa wale wenye miradi pia usimamizi na umakini katika matumizi ya rasilimali fedha hayo yamesemwa na Mh.Mbunge wa Jimbo la Buhigwe FELIX KAVEJURU Hata hivyo amewaomba na kuwakumbusha waheshimiwa madiwani kusimamia miradi inayotekelezwa kwenye kata zao kwani wao ndiyo wenye viti wa maendeleo katika kata zao bila kuwa na wasiwasi.
Wakati hayo yakiendelea ilibainika kuwa kuna walimu walihamishwa vituo vya kazi na kupangiwa vituo vingine ila bado hawajaenda kwenye vituo vyao vipya vya kazi na kutoa agizo kuwa walimu hao waende kwenye maeneo yao ya kazi mapya waliopangiwa haraka iwezekanavyo kauli hiyo ilitolewa na Mh VENANCE KIGWINYA mwenyekiti wa kamati.
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya buhigwe ALPHONCE I HAULE amewataka wataalamu kuwa makini na wakali kwenye usimamizi wa miradi na utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia kanuni na taratibu kwa usawa na ubora unaotakiwa ili kuleta tija katika kazi za halmashsuri
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz