Buhigwe, Kigoma
Kamati ya Fedha Mipango na Uongozi ya Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe leo Septemba 7, 2023 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua Miradi mbali mbali wilayani hapa yenye Dhamani ya Takribani Bilioni 2.
Akizungumza kwenye Ziara hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Venance Kigwinya amesisitiza kuhakikisha wataalamu wanatoka ofini na kukaa kwenye miradi ili kuongeza usimamizi na ubora wa Miradi mbali mbali inayotekelezwa bila kuwaachia Walimu, Waganga,Kamati na wakandarasi.
Awali Kamati hiyo ilifanya Ukaguzi kwenye Miradi inayotekelezwa kwenye Shule ya Sekondari Munanila inayohudumia wanafunzi wa Kidato cha Tano na wanafunzi wa kutwa ambapo Jumla ya Madarasa Manne yenye dhamani ya Tsh. Milioni 104 Na Vyoo vyenye Matundu 8 vyenye Thamani ya Tsh. Milioni 8.8 pamoja na Ujenzi wa Bweni Moja lenye Dhamani ya Tsh. Milioni 136 na kufanya Jumlaya ya Miradi inayotekelezwa hapo kuwa Jumla ya Tsh. 248.8 Ambapo Miradi yote ipo kwenye hatua mbali mbali na uteklezaji wake unatarajiwa kukamilika Septemba 30 mwaka huu chini ya Mkandarasi. Kamati ilishauri kuongezwa kwa kasi Zaidi na Ubora ili dhamani ya Fedha ionekane
Kamati hiyo baadae ilifanya ziara kwenye Zahanati ya Mkatanga inayojengwa kwa nguvu za wananchi ambapo jumla ya gharama zilizotumika kufikia hatua ya lenta ni Tsh. Milioni 40 ambazo ni nguvu za wananchi pekee. Kamati imeendelea kusisitiza Juhudi Zaidi kufanyika na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji katika upatikanaji wa Fedha kwa ajili ya ukamilishaji kwa mapato ya ndani na vyanzo vingine. Pamoja na hayo Kamati hiyo imetoa pongezi kwa wananchi wa kijiji ya Mkatanga kupitia Uongozi wa Kijiji chini ya Mwenyekiti wao ambaye amekuwa ni chachu ya kusimamia upatikanji wa huduma za Afya kijijini hapo kwa namna ambavyo amehamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa Zahanati hiyo.
Baadae kamati ilitembelea Ujenzi wa Nyumba ya makazi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe unaogharimu Tsh. Milioni 120 kutoka Serikali kuu ambapo Ujenzi huo upo kwenye Hatua ya Kufunga Lenta huku miundombinu ya umeme ikiendelea kuwekwa. Kamati imeendelea kusisitiza ubora, ufanisi, kazi na dhamani ya Fedha kuonekana ili huduma hiyo muhimu kwa Mtumishi nambari moja wa Halmashauri ipatikane kwa wakati ili kuongeza tija ya utendaji kazi
Takribani Mita 400 kutoka unapotekelezwa Mradi wa Nyumba ya Makazi ya Mkurugenzi Mtendaji ndiko ilipo Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe na Hatua chache kutoka hapo ndipo unakotekelezwa Mradi wa Jengo la kupumzika akina mama wajawazito wakati wakisubiri kujifungua ambapo kasi ya Ujenzi huo unaotekelezwa kwa hisani ya Dr. Eise, kwa ufadhili wa fedha kutoka Antonius Development Fund Ambao una takribani dhamani ya Zaidi Tsh. Milioni 100 Unaendelea na unatarajiwa kukamilika Septemba 30 mwezi huu. Akiwawakilisha akina mama kwa furaha kubwa Mhe. Elesi Gwoma, Diwani na Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ameshukuru namna ambavyo huduma hiyo itapunguza adha na vifo vya akina mama wilayani hapa.
Baadae kwenye Kijiji cha Buhigwe unapofanyika ukarabati mkubwa wa Jumla ya Madarasa 12 wa Shule ya Msingi Buhigwe, Kamati ilipata nafasi ya kukagua na kushauri kasi na ubora kwenye utekelezaji wake.
Ziara kwa kamati hiyo ilihamia kwenye Tarafa ya Muyama ambapo miradi mbali mbali inatekelezwa huko ikiwepo soko la Muyama Kwenye kwenye Kijiji cha Nyanga, Kata ya Muyama Ambapo utekelezaji wake umekamilika isipokuwa baadhi ya miundombinu ya umaliziaje ambapo kamati ilisisitiza changamoto zote kufanyiwa kazi ili kuwezesha matumizi mazuri ya soko hilo na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
Kamati ilitembelea Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bweni kwa Watoto wenye Mahitaji maalumu Katika shule ya Msingi Muyama ambapo mradi umefikia hatua ya umaliziaji na awali ulitengewa milioni 80 na sasa serikali imeongeza Milion 55 hivyo kufanya Jumla ya Tsh. Milioni 135 kukamilisha mradi huo . Akisoma Taarifa ya Utekelezaji, Mwl. Mkuu wa Shule hiyo Stella Shayo amesema kuwa Pamoja na Changamoto mbali mbali lakini wamesimamia vyema chini ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na wanataraji kukamilisha kwa wakati ili Watoto wenye mahitaji maalumu waanze kupata huduma hiyo shuleni hapo ambao jumla ya Watoto 160 watahudumiwa hapo pindi mradi huo utakapokamilika.
Mwisho kamati ilienda katika Kata ya Kajana kwenye Kijiji cha kajana inakotekelezwa mradi wa Josho lenye dhamani ya Tsh. Milioni 23 kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambalo limeshakabishiwa kwa ajili ya matumizi ambapo baada y ahapo Mita 500 ndiko kilipo Kituo cha Afya Kajana Kilichotengewa Tsh. Milioni 500 ambapo pia ujenzi wa Majengo 6 upo kwenye hatua mbali mbali hasa umaliziaji ambapo baada ya ukaguzi Kamati ilishauri mambo mbali mbali hasa ushirikishwaji wa wana-kamati katika utekelezaji wa miradi ili kuongeza uwazi, ufanisi na umiliki wa mradi kwa jamii.
Kwa niaba ya Kamati hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Venance Kigwinya amepongeza wana-kamati na wataalamu kwa ushirikiano na kusisitiza taratibu kufuatwa katika kila hatua ya utekelezaji wa miradi ya serikali. Mwisho hakuacha kuendelea kupongeza na kushukuru juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna inavyoona huduma bora kwa wananchi wa Buhigwe kama kipaumbele cha serikali yake.
Ikumbukwe Hivi karibuni Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe imepokea Fedha Zaidi ya Tsh. Bilioni 3 ili kutekeleza Miradi mbali mbali kama Umaliziaji wa Majengo ya Shule, Vituo vya Afya, Zahanati, Ujenzi wa uzio nk ambapo utekelezaji wake umeanza mara moja
Silas, J
Kaimu Afisa Mawasiliano Serikalini (W)
Buhigwe
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz