Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Mheshimiwa Charles A. Pallangyo ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kwa namna walivyofanya kazi kwa ushirikiano na bidii hatimae kupata hati safi kwa miaka minne mfululizo.
Aidha Mheshimiwa Charles amewaagiza Wataalam wa Halmashauri hii kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na Waheshimiwa Madiwani ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi kwa kufanya mikutano ya hadhara ngazi ya vijiji na mabaraza ya kata.
Katibu Tawala ameyasema hayo leo asubuhi katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Buhigwe.
“Hakikisheni hoja za miaka ya nyuma zinajibiwa/zinafungwa mapema na kuwasilishwa kwa mkaguzi wa nje kwa ushirikiano wa ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).” Aliongeza Mheshimiwa Charles.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz