• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za ofisi |
Buhigwe District Council
Buhigwe District Council

Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Msingi Mkuu
    • Mpango Mkakati
  • Utawala
    • Muundo Wa Utawala
    • Idara
      • Utawala Na Utumishi
      • Mipango, Takwimu Na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha Na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Secondari
      • Maji
      • Mifugo Na Uvuvi
      • Ardhi Na Maliasili
      • Maendeleo Ya Jamii Na Ustawi Wa Jamii
      • Ujenzi Na Zimamoto
      • Kilimo,Umwagiliaji Na Ushirika
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi Wa Ndani
      • Habari Na Mawasiliano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kiutalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Wah. Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao
      • Kuonana na Mhe.Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayotarajiwa Kufanywa
    • Miradi Inayoendelea Kufanywa
    • New Planned Project
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Other Fomu
    • MpangoKazi
    • Baraza-Madiwani
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Hongera sana Dkt. Philip Isdor Mpango kwa kuthibitishwa kuwa Makamu wa Rais Tanzania Bara

Posted on: March 30th, 2021

Leo Rais Samia Suluhu Hassan amewasilisha mapendekezo ya jina lake kuwa makamu wa Rais katika kikao maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na baadaye jina hilo kuwasilishwa bungeni na kupitishwa kwa kura 363 sawa na asilimia 100 ya kura zote zilizopigwa.

Baada ya kupokea jina lake, Spika Job Ndugai alilitangazia bunge jina hilo lililopendekezwa na Rais Samia.

Baada ya kupokea jina lake, Spika Job Ndugai alilitangazia bunge jina hilo lililopendekezwa na Rais Samia.

Mara baada ya tangazo hilo bunge lililipuka kwa shangwe.

Bwana Mpango alikuwa waziri mwandamizi katika serikali ya hayati John Magufuli akihudumu kama waziri wa fedha.

Na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, asilimia 50 ya wabunge wanatakiwa kuukubali uteuzi huo ili kuthibitishwa.

Kabla ya jina hilo kuwasilishwa bungeni hii leo, kwanza liliwasilishwa katika Kamati kuu ya chama tawala CCM na kuthibitishwa.

'Nimepigwa na butwaa'

Mara tu baada ya jina lake kusomwa Spika Ndugai alimpatia Mpango muda wa kujieleza ndani ya Bunge.

Mpango akaeleza kuwa hakujua chochote juu ya uteuzi huo na kwamba alipigwa na butwaa.

''...Hii ni heshima kubwa sana, sikuwahi kuota (kama nitaipata)...Mpaka Naibu Waziri wangu akiwa anajibu maswali asubuhi hapa, nilikuwa nafikiria majukumu yangu yanayonikabili ikiwemo mishahara ya wabunge ambayo baadhi imechelewa mpaka asubuhi hii. Nimepigwa na butwaa..."

Phillip Mpango ni nani?

Dkt. Philip Mpango alikua Waziri wa Fedha na Mipango katika Serikali ya Awamu ya Tano, ameteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la Rais John Magufuli.

Mwaka 2015 alikua mbunge wa kuteuliwa.

Bwana Mpango ni mzaliwa wa Kigoma, baba yake ni marehemu Isidori Nzabhayanga Mpango, ambaye alizaliwa Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Kasulu.

Dkt. Mpango alizaliwa hapo hapo Kasumo na ni kaka mdogo wa Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanganyika Magharibi - Kasulu mkoani Kigoma, Dk Gerard Mpango.

Dk Mpango ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu ya uchumi.

Kuanzia miaka ya 1990 hadi 2000, alifanya kazi akiwa mhadhiri mwandamizi wa uchumi katika kitivo cha Biashara (sasa Shule ya Biashara) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Alikuwa akifundisha "Microeconomics", "Macroeconomics" (kwa mwaka wa pili) na "Public Finance" kwa mwaka wa tatu na kozi za uzamili. (Kwa tafsiri yangu, Uchumi mdogo, Uchumi mkubwa na masuala ya Fedha za umma.)

Amewahi kuwa Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Mkuu wa Kamati ya kumshauri Rais Jakaya Kikwete wakati huo kuhusu masuala ya uchumi, Katibu binafsi wa Rais anayeshughulikia masuala ya uchumi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, kabla ya kuhamishiwa Tume ya Mipango, Ofisi ya Rais.

Nyadhifa hizi zote amezishika wakati wa utawala wa Kikwete.

Hayati Magufuli alipoingia madarakani alimteua kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baada ya siku chache akateuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Katika uchaguzi wa mwaka 2020 alishinda kiti Cha ubunge jimbo la Buhingwe.

Kisha kuteuliwa tena kuwa waziri wa fedha na Mipango.


Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAILI - 04.07.2023 June 23, 2023
  • KILA KHERI DARASA LA SABA September 12, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA - OKTOBA 2023 October 09, 2023
  • TANZIA February 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED BUHIGWE ATEMBELEA VITUO VYA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA.

    May 05, 2025
  • MATOKEO 2024 WALIMU NA WANAFUNZI WAPONGEZWA.

    April 17, 2025
  • BABA ASKOFU EMMANUEL BWATA AITIKIA WITO WA MKURUGENZI BUHIGWE.

    April 14, 2025
  • SHEREHE YA KUWAAGA WATUMISHI NA KUWAKARIBISHA WATUMISHI BUHIGWE YAFANA.

    April 13, 2025
  • Angalia zote

Video

Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe kuanza kutoa huduma za Afya
Video Zaidi

Kurasa Za Karibu

  • Kuhamisha Mwanafunzi
  • Tovuti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
  • FFARS USER GUIDE
  • PlanRep Documentation
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • Kata Zetu
  • Wahe. Madiwani
  • BEMIS

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Bunge La Tanzania
  • Ikulu
  • Bodi Ya Manunuzi na Ugavi
  • Wizara ya Ardhi
  • Wizara ya Elimu, Sayansi

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi

    Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe

    Simu Ya Mezani: 0282988460

    Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333

    Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma
    • Mwanzo

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Buhigwe. Haki zote zimehifadhiwa