Zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya wafanya biashara wadogo wilayani Buhigwe, mkoani Kigoma, limeeendelea leo asubuhi ofisini kwa Mkuu wa Wilaya kwa kuwapatia wafanya biashara baadhi waliohudhuria zoezi hilo, huku wito ukitolewa kwa wafanya biashara wadogo ili wajitokeze kwa wingi kuchukua vitambulisho hivyo.
Mheshimiwa Ruteni Kanali Michael M. Ngayalina, Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe akizungumza na wafanya biashara wadogo Wilayani hapa amesema, Serikali haitarajii kukutana na mfanya biashara Ndumila kuwili.
Wako ambao wataandikishwa kama wafanya biashara wadogo na wako walioandikishwa na TRA watakuwa na leseni toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri, na watakuwa wanalipa mapato TRA.
"Kwa hiyo tunagemea kupata wafanya biashara wa aina mbili ambao ni mfanya biashara mdogo na mkubwa. Hatutegemei kupata mfanya biashara aliyekatikati kama Ndumila kuwili" amesema Mhe.Mkuu wa wa Wilaya.
Ameongeza Serikali imejipanga kuelimisha wananchi kuhusu elimu ya mlipa kodi ili iweze kufikia malengo tarajiwa.
Akihamasisha wafanya biashara hao (wadogowadogo), Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Bwana Anosta L. Nyamoga amesema, elimu ya mlipa kodi ndio itakayomweka mfanya biashara sehemu salama, hivyo fanyeni biashara zenu kwa bidii ili mitaji yenu ikue huku mkivitumia vitambulisho hivyo kwa umakini sana kwani sheria kali zitachukuliwa dhidi ya mfanya biashara atakayebainika amekiuka matumizi ya vitambulisho hivi.
"Watu wanashindana kukwepa kodi, wakati mataifa mengine yaliyoendelea yanashindana kulipa kodi..hili halikubaliki hata kidogo"alisema Nyamoga, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.
Kwa upande wao wafanya biashara wadogo wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwapatia vitambulisho kwakuwa wako huru sasa kufanya biashara zao.
"Usipokuwa na elimu ya mlipa kodi kila kukicha utakuwa unailalamikia Serikali, huku ukipoteza fursa katika nafasi hiyo,
Kuna mbinu nyingi zinazotumiwa kukwepa kodi, nitakuwa mstari wa mbele kuhamasisha wafanya biashara wenzangu kwa kuwapa elimu ili walipe kodi ya Serikali na sio kukwepa".”. Alisema mmoja wa wafanya biashara hao.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz