Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe Ndg George Emanuel Mbilinyi Leo Juni 7,2024 amekutana na viongozi wawakilisha wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) ofisini kwake.
Lengo la ugeni huo ni kushirikiana kukarabati kituo Cha rasilimali za Kilimo Mifugo na Uvuvi Kata ya Kibwigwa katika Halmashauri ya Buhigwe,
Akiongea katika ukaguzi wa kituo hicho Mwakilishi wa FAO Bw. Charles Tulahi amesema kuwa Shirika linalenga kutumia kiasi Cha shiling million 35,87880 katika ukarabati wa kituo hicho.
Kituo hicho kitakapo kamilika kinatarajiwa kutoa huduma za mafunzo ya Kilimo Mifugo na Uvuvi ikiwa ni pamoja na mashamba Darasa ya Mazao mbali mbali,Malisho ya mifugo na mabwawa ya ufugaji Samaki kwa lengo la kuongeza Tija kwa wakulima na wafugaji.
Aidha katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Buhigwe Bw. Mbilinyi Amewashukuru Shirika la FAO kwa kuboresha kituo hicho na kuleta Tija katika Halmashauri yetu na kuinua kipato Cha wakulima na wafugaji pia Amewashukuru viongozi wa Kijiji Cha Kibwigwa kwa kutenga eneo kwaajili ya uwekezaji huo.
Wakati hayo yakiendelea pia Shirika la FAO limetoa mafunzo ya Kilimo hifadhi na lishe kwa wataalam wa kilimo 17, wakulima 647 na kugawa vitendea kazi mbali mbali ikiwemo computer mpakato, overall, bomba la kunyunyiza dawa na mashine za kurahisisha upandaji mimea mbali mbali.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz