Kamati ya lishe Wilaya ya Buhigwe imefanya ufuatiliaji na kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya lishe bora kwa mtoto chini ya miaka miwili pamoja na mama mjamzito kupitia mradi wa Mtoto Mwerevu.
Mwakilishi wa mradi huo wa Mtoto Mwerevu Nd. Zidiel Mzirai alikutana na wajumbe wa kamati katika ngazi ya kijiji ili kubaini changamoto wazakutana nazo na namna ya kuzitafutia uvumbuzi.
Pamoja na hili aliwakumbusha malengo makuu ya Mradi wa MTOTO MWEREVU.
Miongoni mwa malengo ya mradi huu ni kupunguza udumavu kwa watoto chini ya miaka miwili.
Ndg. Zidieli Mzirai alitowa elimu juu makundi ya chakula elimu ambayo CHW wanatakiwa kufundisha kwajamii ili kuweza kuondoa udumavu kwajamii husika.
Aina ya chakula lishe.
Moja ya lengo la ziara hii ni pamoja na kufuatilia ujazaji wa fomu ambazo zinatumika kufuatilia upimaji na mtiririko mzima wa hali ya udumavu kwa watoto.
Kwa kuzingatia siku 1000 kwa makuzi ya mtoto ni siku zenye umuhimu sana. Siku hizi zinaanza kuanzia mara tu mimba inapotungwa kwa mama majamzito hadi mtoto atakapofikisha miaka miwili.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz