Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt Philip Isidor Mpango leo tarehe 27 mwezi Agosti 2025 amezindua tawi la benki ya CRDB Wilaya ya Buhigwe.
Akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua tawi hilo na kukabidhi madarasa mawili katika Shule ya Sekondari Kibande amewaasa Wananchi kuwa na nidhamu ya pesa kwa manufaa ya familia na nchi kwa ujumla kwa kutumia pesa kwa malengo yaliyokusudiwa
Aidha ameongezea kwa kuwaasa kutunza na kulinda amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa kuchagua Rais,Wabunge na Madiwani na kujitokeza kwa wingi kutimiza haki ya msingi ya kuchagua viongozi muda utakapowadia na pia amewahimiza kutunza mazingira na kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya nchi.
Sambamba na hilo amewapongeza viongozi wa kigoma na Wilaya ya buhigwe kwa ujumla kwa uchapakazi makini wenye kuleta maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ameishukuru Benki ya CRDB kwa huduma bora wanayoitoa kwa Jamii.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB AbdullMajid Lusekela amesema kuwa benki ya CRDB imefanikiwa kufikia Wilaya 6 za Mkoa wa Kigoma na kutoa huduma kwa lengo la kuwasaidia Wananchi na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuweka mazingira mazuri ya kiuchumi.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz