Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango amefanya ziara ya kutembelea ujenzi wa mradi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kahimba wilaya ya Buhigwe ambayo tayari imeanza kutumika.
Dkt Mpango amefanya ziara hiyo baada ya kuhudhuria Maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani kwa Kanda ya Magharibi lililolenga kujadili mchango na Ushiriki wa wanawake katika Matumizi ya Nishati Safi na Utunzaji wa Mazingira, ambalo limefanyika katika Ukumbi wa NSSF, Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Akizungumza katika ziara hiyo ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe chini ya Mkurugenzi wake Ndug George Emmanuel Mbilinyi,Mkuu wa Wilaya,Kanali Michael Ngayalina na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Tobias Andengenye na watumishi wote kwa kusimamia vizuri mradi huo ambao umeanza kutumika kupokea Wanafunzi wa kidato cha kwanza.
Aidha ameongezea kwa kuwaasa Wanafunzi waliochaguliwa katika shule hiyo kusoma kwa bidii ili kutengeneza viongozi wasomi na hodari wa baadae.
Sambamba na hilo amewataka Wananchi wa maeneo ya jirani na shule hyo kutunza mazingira ili kuzitendea haki fedha zilizoletwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kujenga shule hiyo na kuwa waadilifu kwa kuwaaacha watoto hao kusoma bila kuwafanyia udanganyifu.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz