Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George Emmanuel Mbilinyi amewahimiza Watendaji wa kata na vijiji Wilayani humo kutambua na kutimiza wajibu wao.
Ameyasema hayo leo tarehe 10 Septemba 2025 wakati akizungumza nao katika kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za Halmashauri hiyo.
Aidha amewasihi kubaini rasilimali zilizopo katika maeneo yao na kusimamia miradi ya maendeleo kwa ufanisi.
Naye Afisa Utumishi Wilaya ya Buhigwe Hamza Seif amewataka Watendaji hao kufanya kazi kwa kufuata kanuni na sheria za utumishi wa umma.
Sambamba na hilo amewasihi kuboresha miundombinu katika maeneo yao ya kazi.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz