Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George Emmanuel Mbilinyi amewataka wakandarasi wa kampuni ya ujenzi ya Micrence company limited wa shule ya Sekondari Biharu kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.
Akizungumza katika kikao kilichofanyika leo tarehe 02 mwezi Januari mwaka 2025 na Kampuni ya Micrence company Limited Wakuu wa Idara ya Elimu Sekondari,Msingi,Manunuzi,Sheria na Mhandisi wa ujenzi katika ofisi za Halmashauri zilizopo Wilayani hapa amesema kuwa mradi huo ni muhimu kukamilika kwa wakati ili kuboresha mazingira rafiki kwa Wanafunzi kujifunza.
Mkurugenzi Mtendaji ameitisha kikao hicho baada ya mradi huo kusuasua na kutofanyika kwa muda uliopangwa kwenye mkataba.Mradi huo ni ujenzi wa block mbili wenye vyumba vinne vya madarasa,Nyumba ya Walimu two in one,Mabweni mawili na vyoo matundu 10 ukigharimu kiasi cha Shilingi Milioni 508,000,000.00
#buhigwefahariyetu #2025kaziiendelee