Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George Emmanuel Mbilinyi akiongozana na Wakuu wa Idara mbalimbali amefanya ziara katika kijiji cha Bulimanyi kilichopo kata ya Nyamugali katika Wilaya ya Buhigwe ikiwa na lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali za Wananchi na kuzungumza nao kuhusu masuala mbalimbali ya kimaendeleo.
Akizungumza na Wananchi hao amewashukuru Wananchi wote waliojitokeza katika mkutano huo pamoja na kuwapongeza wale wote waliotoa changamoto ambazo kwa pamoja wamezitolea ufumbuzi.
Ameongezea kwa kuwaahidi kumaliza kero ya soko la Nyamugali ambalo serikali imetenga Milioni 35 kwa ajili ya kufanya maboresho mbalimbali katika soko hilo pamoja na kuwasihi kuunga mkono mpango mkakati wa chakula mashuleni.
Sambamba na hilo ametoa rai kwa Wananchi wote kujitokeza kwa wingi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa kuchagua viongozi mbalimbali ikiwemo,Madiwani,Wabunge na Rais unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu wa 2025.
Kwa niaba ya Wananchi wa kata ya Nyamugali Diwani Arudon Kisigaye amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji pamoja na timu yake kwa kuwatembelea na kutatua changamoto zao.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz