Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George Emmanuel Mbilinyi amewasihi wafugaji wote wa wilaya hiyo kufanya utambuzi na usajili na kuchanja mifugo yao.
Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 9 Oktoba 2025 wakati akikabidhi vishikwambi kwa maafisa ugani-mifugo wote wa wilaya ya Buhigwe vilivyotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikiwa na lengo la kufanya utambuzi,usajili,na uchanjaji wa mifugo.
Aidha ameongezea kwa kuwaasa maafisa ugani hao kufanya kazi kwa bidi kwa maendeleo ya taifa na kutumia vishikwambi hivyo kwa lengo lililokusudiwa na kuvitunza vishikwambi hivyo.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz