Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George Emmanuel Mbilinyi tarehe 13 mwezi Januari 2025 ametembelea Shule mbalimbali za Sekondari na Msingi katika Wilaya ya Buhigwe ikiwemo Shule ya Sekondari ya Wasichana Kahimba ambapo inatarajiwa kupokea Wanafunzi 100,Kilelema,Katundu kwa ajili ya kupokea Wanafunzi pamoja na kukagua mahudhurio yao.
Zoezi la kupokea Wanafunzi limeanza rasmi siku ya Jumatatu tarehe 13 mwezi Januari 2025 kwa msimu huu mpya wa masomo huku Wanafunzi wakiendelea kuripoti kwa wingi.
Aidha amesisitiza kuwepo kwa mipango madhubuti ya Uhamasishaji wa Wazazi na Walezi ili kuleta watoto kuwasili shuleni kwa wakati.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz