Mhe:Col Michael Masala Justine Ngayalina Mkuu wa wilaya ya ameongoza zoezi la ugawaji wa zawadi kwa wasimamizi bora wa miradi inayotekelezwa katika shule za awali na msingi na sekondari kwa kumaliza utekelezaji wa miradi kwa wakati na kutumia vizuri rasilimali fedha hivyo kufanya miradi kukamilika kwa wakati na ipasavyo: hata hivyo amesema tukisimamia miradi ya serikali inayotekelezwa katika shule zetu vizuri tutambue kwamba hata miradi yetu binafsi tunaweza kuisimamia vyema
Si hivyo tu, ametoa zawadi kwa shule zilizofanya Vizuri kwa ufaulu kitaifa,mkoa wilaya hata kimasomo kwenye mitihani ya kidato cha nne, darasa la saba,na darasa la pili; Ikiwa lengo ni kutoa hamasa kwa walimu na kuwapa motisha wa kuendelea kufundisha na kupenda mazingira yao ya kazi . Hata hivyo ametoa wito kwa walimu kutafuta juhudi za pekee kuendelea kufanya vizuri katika ufundishaji ili kuongeza ufaulu zaidi na zaidi
Pia, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndug Alphonce Innocent Haule amewapongeza walimu kwa juhudi zao zote katika ufundishaji wao na kuwaomba kuendelea kuboresha utoaji elimu katika shule zao za awali na msingi na sekondari si hivyo tu amewakumbusha walimu wote wanaopewa dhamana ya kusimamia miradi inayotekelezwa katika shule Zao kujitoa kwa moyo wa dhati kusimamia miradi hiyo kwa kuzingatia kanuni sheria na taratibu zote za usimamizi wa miradi pia za kiutumishi na kusisitiza kusimamia vyema haswa matumizi ya rasilimali fedha
Akiwasilisha mada Ndug Godwin sanane Nsemwa Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi amewakumbusha wasimamizi wote wa miradi kuwa manunuzi yote ya vifaa yatafanyika kwenye mfumo wa NeST na si vinginevyo Hata hivyo Amewakumbusha kuzingatia kanuni na taratibu zote za manunuzi wakati wa manunuzi ya vifaa vyote katika utekelezaji wa mradi
Hali kadhalika, Ndugu Justin Njuu Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu amesema wasimamizi wote wa miradi inayotekelezwa katika shule zote ni maafisa Masuhuli wasaidizi hivyo wanapaswa kutekeleza miradi hiyo kwa kuzingatia mipango na bajeti za miradi mipya na miradi ya kumalizia, lakini pia amawaasa kuwashirikisha wananchi na viongozi wote wanaozunguka maeneo mradi unapotekelezwa
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz