Mhe Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Col Michael Masala Justine Ngayalina akiwa kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa gari ya kubebea wagojwa (Ambulance) ahimiza matumizi sahihi ya magari hayo.
Akiwasilisha taarifa ya mapokezi ya gari hilo Dkt Innocent Mhagama Mganga Mkuu wa Wilaya amesema Mpaka sasa Halmashauri inajumla ya Magari manne (4) yakubebea wagonjwa kati ya hayo Magari matatu (3) yanafanyakazi ( Hospitali ya Wilaya,Kituo cha afya Muyama na Janda) hata hivyo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuikumbuka Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kwa kuipatia Msaada wa Gari jipya aina ya TOYOTA LAND CRUISER(Ambulance)
Akitoa shukurani za dhati za wanabuhigwe Mhe Col Michael Masala Justine Ngayalina Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa upendo mkubwa na uchapakazi uliotukuka kwani hatukutengemea makubwa haya lakini sasa awamu ya sita ya mama imefanya Zaidi si hivyo ameshukuru sana kwa kutupatia gari hilo kwani litapunguza adha kubwa za wananchi sio tu wa mwayaya bali wa buhigwe nzima pia tutapunguza vifo vya mama na mtoto
Akikabidhi gari hilo kwa mfawidhi wa kituo hicho Ndugu Edithi Kimondo ameonya matumizi mabaya ya gari hilo na si vinginevyo. Aidha amehimiza upatikanaji wa gari masaa 24 kituoni hapo lengo ni kuhakikisha huduma inapatikana kwa usahihi.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz