Kikao hicho kimefanyika Mei 31,2024 katika ukumbi wa utawala Hospital ya Wilaya ya Buhigwe kikiwa na lengo la kwenda kuhamasisha wazazi na walezi kuchangia vyakula mashuleni.
Walioshiriki kikao hicho ni Weo's Dhro Elimu Msingi na Sekondari kwakuwa wao wanahisika kwa ujumla wao kutoa Elimu na uhamasishaji katika jamii au wazazi na walezi wa watoto ili wajue umhimu wa wanafunzi kupata chakula mashuleni.
"Ndugu washiriki; Sote tunapaswa kufahamu lishe ni suala mtambuka na utapiamlo katika jamii ni matokeo ya mkusanyiko wa matatizo mengi. Matatizo hayo yanaweza kusababishwa na ulaji duni na mtindo wa maisha usiofaa, maradhi mbalimbali, kutokuwa na uhakika wa chakula, matunzo duni ya akina mama wajawazito na watoto, mazingira machafu, rasilimali haba na mgawanyo usiokuwa na uwiano sahihi kijinsia, umaskini wa kipato, machafuko ya kisiasa na hata sera zisizotambua umuhimu wa lishe kwa maendeleo ya mwanadamu na taifa kwa ujumla wake.
Kila familia inapaswa kufahamu umuhimu wa lishe bora. Hii ni kwasababu takriban nusu ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano kila mwaka hutokana na ukosefu wa lishe bora, unaosababisha kudhoofika kwa kinga mwili hivyo kupelekea mwili kushindwa kupambana na magonjwa. Vilevile lishe duni huwaweka wanawake wajawazito katika mazingira hatarishi yanayoweza kusababisha kujifungua watoto njiti, Watoto wafu, watoto wenye mtindio wa ubongo au hata kuharibika kwa mimba na vifo vya akina mama wakati au baada ya kujifungua.
Wataalam wanatuambia kuwa watoto waliopata huduma bora na sahihi za lishe, katika kipindi cha siku 1,000 za mwanzo wa uhai wao (kwa maana ya miezi tisa ya mimba na mpaka kufikia umri wa miaka miwili baada ya kuzaliwa) wanapata faida zitakazodumu katika maisha yao yote ikiwa ni pamoja na maendeleo mazuri ya ukuaji wa ubongo, uwezo mzuri wa kukabiliana na maradhi, uwezo mkubwa wa akili za utambuzi (higher IQ), uwezo mkubwa na ufanisi.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz