Katika kuadhimisha Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Wilaya ya Buhigwe ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina na Mkurugenzi Mtendaji ndug George E Mbilinyi wamefanya usafi katika maeneo mbalimbali ikiwemo Soko la Kibwigwa.
Akizungumza na Wananchi Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe amesema kuwa ikiwa ni kumbukumbu ya kupata uhuru kutoka kwa wakoloni Wananchi wote ni jukumu la kila mtu kuweka mazingira safi na salama.
Pamoja na hayo amewaasa Wananchi wote wa Wilaya ya Buhigwe kudumisha Amani na upendo uliopo pamoja na kujali afya zao.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz