Wananchi Wilayani Buhigwe wametakiwa kuacha imani potofu na kujitokeza kwa wingi kujiandikisha muda utakapowadia ili kupatiwa vyandarua vyenye dawa kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa malaria nchini.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael Ngayalina wakati wa kikao kazi cha kuhamasisha zoezi la ugawaji wa vyandarua bila malipo kwenye kila kaya katika Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe.
Aidha ameongezea kwa kuwaasa kutumia vyandarua kwa matumizi yaliyokusudiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si kinyume cha hapo kama baadhi walivyozoea.
Naye mwakilishi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI Bw.Januari Boniventure amewaasa maafisa Afya na Mazingira katika Halmshauri ya wilaya ya Buhigwe kuweka sheria ndogondogo zitakazosaidia Wananchi kuzingatia usafi wa mazingira ili kupunguza kuenea kwa ugonjwa huo.
Kwa upande wake Peter Gitanya kutoka Wizara ya afya chini ya mpango wa taifa wa kudhibiti Maralia amesema kuwa kwa niaba ya Wizara ya Afya agenda ni moja kuhakikisha inatokomeza Malaria nchini ifikapo mwaka 2030.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe Dkt Innocent Mhagama amesema wanatekeleza afua mbalimbali za kutokomeza ugonjwa wa malaria ikiwemo kutoa vyandarua kwa wanawake wajawazito na watoto.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz