Katika kusherehekea sikukuu ya Mwaka Mpya,Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina amewataka Wananchi wa Buhigwe na Watanzania kwa ujumla kuiga mfano wa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani wa kuwakumbuka watoto wenye mahitaji maalumu.Ameyasema hayo leo tarehe 30 mwezi 12 katika hafla ya utoaji wa Zawadi ya vyakula na vifaa mbalimbali kwaniaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vyenye thamani ya shilingi Milioni 1 na Laki 9 katika shule ya msingi Muyama kwa ajili ya Watoto wenye mahitaji maalumu.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmshauri ya wilaya ya Buhigwe George Emmanuel Mbilinyi amesema kuwa Lengo la kutoa vitu hivyo ni kutekeleza agizo la Mh Rais Samia la kutambua umuhimu wa watoto wenye mahitaji maalumu katika msimu huu wa kusherekea sikukuu za mwaka.
Nao baadhi ya wazazi na walezi wa watoto hao Wameishukuru Serikali kwa kutambua mchango wa watoto wenye mahitaji maalumu kwa kuwapatia zawadi ya chakula na vitu mbalimbali.