Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Col. Michael M. Ngayalina ameshiriki zoezi la kupanda miti eneo la Ofisi za Mkurugenzi Mtendaji (W) zilizoko mji wa Bwega wakati wa sherehe za kumbukizi ya miaka 59 ya Uhuru wa Tanganyika.
Akizungumza na Watumishi toka Ofisi ya Mkurugenzi Mhe. Ngayalina amesema ni vyema wakati tunaadhimisha sherehe hii tukumbuke kupanda miti kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho kwani miti ina faida nyingi sana ikiwemo, dawa, matunda, kivuli, mbao, karatasi n.k.
Kwa upande wa watumishi wamefurahi sana kushiriki zoezi hilo wakiwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya na kuahidi kuitunza miti iliyopandwa leo.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz