Katibu tawala wa Wilaya ya Buhigwe Mh Utefta Mahega amewataka Watumishi wa umma Wilaya ya Buhigwe kuzingatia Demokrasia na Utawala bora ili kuendelea kujenga imani kwa Wananchi dhidi ya Serikali yao ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hayo ameyasema leo tarehe 29 mwezi Januari 2025 katika mafunzo ya Elimu ya Uraia na Utawala bora yaliyoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria yaliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George Emmanuel Mbilinyi ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kwa kuleta mafunzo hayo na kuwasihi watumishi hao kutumia mafunzo hayo katika utendaji wao wa kazi.
Joyce Mushi ambaye ni Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na Mratibu wa mafunzo hayo amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo viongozi wa Serikali za Mitaa ili kutatua changamoto na malalamiko katika jamii kwa kuzingatia demokrasia na utawala bora. Aidha ameongezea kwa kuwashukuru.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz