Katika kuadhimisha Siku ya Kichaa cha Mbwa Duhiani hii leo Septemba 28, 2023 Wilayani Buhigwe imefanyika katika kata ya Kibwigwa amabapo Mgeni Rasmi alikuwa Mhe. Col. Michael Ngayalina ambaye Pamoja na kuwaasa Wafugaji na wananchi kuhakikisha wanawachanja mbwa wao ili kuutokomeza ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa lakini alishiriki kuchanja Mbwa dhidi ya Kichaa na Kushiriki kutoa uzazi kwa Mbwa.
Awali akisoma Taarifa ya Kichaa cha Mbwa Wilayani Hapo Ndg. Leonard, Mganga wa magonjwa ya Wanyama alieleza kuwa kwa Mwaka 2022 Mtu mmoja alifariki kwa kuumwa na Mbwa mwenye Kichaa na kuwaeleza wananchi juu ya madhara na dalili za Kichaa cha mbwa
Akizungumza katika maadhimisho hayo Col. Ngayalina amewataka wananchi kuondoa dhana kuwa waganga wa Kienyeji wanaweza kuponya ugonjwa wa kichaa cha mbwa kwa kunyonya kidonda cha Mwadhirika bali njia bora ya kupambana na kichaa cha mbwa ni kuhakikisha mbwa wanapata chanjo kwa wakati
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg. Alphonce Haule amewataka wananchi kutopuuzia chanjo na utunzaji wa Wanyama hao ambao ameeleza kuwa wamekuwa wakisaidia si kwa shughuli za ulinzi na uwindaji bali wamekuwa wakitumika kama mapambo pale wanapotunzwa vyema na kuongeza kuwa Tanzania na Dunia inatumia gharama kubwa kukabiliana na ugonjwa huo ambapo kwa kutokomezwa gharama hizo zinaweza kuokolewa na kufanya shughuli nyingine zenye tija.
Jumla ya Mbwa 128 wamepatiwa chanjo bure katika siku hiyo Katika kata ya Kibwigwa ambapo wataalam wa Halmashauri hiyo wamepiga kambi kwa siku nzima Mkuu wa Wilaya ameongoza Uchanjaji huo.
Mwisho Mhe. Ngayalina alishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe. DKT Samia Suluhu Hassa ambayo kwa upekee imeona ni vyema kutoa huduma hiyo kwa wananchi ili kuondokana na ugonjwa huo wenye madhara hasi kwa Jamii.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz