Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kanali Michael Ngayalina amewataka Wananchi wa wilayani humo kutumia nishati safi ya kupikia ya ruzuku iliyoletwa na serikali kwa ajili ya kutunza mazingira.
Hayo ameyasema wakati akizungumza na Wananchi mbalimbali alipokuwa akikabidhi mitungi ya gesi iliyoletwa na Wakala wa Nishati vijijini (REA) wakishirikiana na kampuni ya Oryx yenye punguzo la bei ikiwa ni juhudi za Serikali ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani katika kuhakikisha Wananchi wote wanatumia nishati safi ya kupikia.
Aidha kwa niaba ya Wananchi wa Buhigwe amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassani na makamu wa rais Dkt Philip Mpango kwa kuwapatia nishati ya gesi yenye bei nafuu ambayo inamuwezesha kila mwananchi kuimudu.
Kwa upande wake Mhandisi wa Mradi huo kutoka Wakala wa Nishaji vijijini (REA) Ramadhani Mganga amewaasa Wananchi wote kuhakikisha wanaacha kutumia nishati ya mkaa na kuni ya kupikia na kuhamia katika nishati safi ya kupikia ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sera yake ya utunzaji wa mazingira.
Aidha ameongezea kwa kusema kuwa zoezi hili la uuzaji wa nishati safi ya kupikia kwa mkoa wa Kigoma linahusisha jumla ya mitungi 19530 ya gesi.
Melesiana Josiah na Amos Kavejuru ni Wakazi wa Wilaya ya Buhigwe ambao wameishukuru Serikali kwa kuwapatia nishati hyo ya ruzuku ambayo itaenda kupunguza uchafuzi wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz