Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh Tobias Andengenye amewaasa watumishi wa umma kutunza vifaa kazi wanavyopewa na Serikali kwa malengo yaliyokusudiwa.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vitendea kazi ikiwemo magari mawili kwa ajili ya usimamizi wa mazao ambayo yametolewa kwa ofisi ya Mkoa wa Kigoma na Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe iliyofanyika katika ofisi za Mkoa huo.
Aidha amesema kuwa mpango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuona kuwa Tanzania inakuwa ghala la chakula na hivyo kuifanya kuwa fursa ya kulisha Afrika na dunia kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndugu George E Mbilinyi ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Mh Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuwapatia vitendea kazi pamoja na kuahidi kuvitunza vifaa hivyo.
“Tumepokea gari hili ambalo tunaenda kulitumia kwenye idara ya Kilimo ufuatiliaji, na kwa nafasi ya pekee sana tunamshukuru Mh Rais kwa hiki ambacho amekifanya,ametuongeza nguvu ya kufuatilia na kuwahudumia wakulima wake wa Buhigwe na kwa namna ya pekee tumepokea maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa na Katibu tawala utunzaji na matumizi ya gari yaweze kwenda sahihi kwa malengo yaliyokusudiwa”Alieleza Mbilinyi
Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe imepokea gari hilo kwa awamu ya kwanza ikiwemo taarifa ya kuwa Halmashauri nyingine kupata kwa awamu ya inayofuata kutoka Wizara ya Kilimo kwa ajili ya Usimamizi wa Mazao chini ya Ajenda 10/30 ya Kilimo ni biashara
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz