Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof. Joyce Ndalichako amefanya ziara yake leo Wilayani Buhigwe, ambapo alipata nafasi ya kutembelea shule ya sekondari Janda iliyoko kata ya Janda wilayani hapa.
Akizungumza na Wananchi wa Kata hiyo,baada ya kupokea taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Janda Prof. Ndalichako amesema Serikali kupitia programu ya Lipa kulingana na matokeo (EP4R) imetoa shilingi milioni 993 na laki mbili tangu mwezi Jnauri mwaka huu kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu kama vile Mabweni, maabara, madarasa, nyumba za walimu na matundu ya vyoo katika shule za msingi na sekondari Wilayani Buhigwe.
Aidha Mhe. Waziri amewapongeza Mtendaji wa kata, Mhe. Diwani, wazazi na uongozi wa shule kwa jitihada wanazozionesha katika kuhakikisha watoto wanapata elimu bora. Pongezi hizo zimetolewa baada ya kuona jitihada za wananchi kujenga vyumba vya madarasa viwili, maabara na nyumba za walimu mbili, ambapo amewaunga mkono wananchi kwa kutoa ahadi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala.
“(Nawapongeza wazazi na Boodi ya Shule kwa juhudi zenu amabazo kwa asilimia kubwa zimechangia maendeleo ya Shule hii, mmekuwa waanzilishi wa shughuli za ujenzi wa miundombinu ya shule na serikali imekuwa ikisaidia umaliziaji wa pale mnapokuwa mmekwama. Kwakweli mmekuwa mfano wa kuigwa na ninaomba juhudi hizo ziendelee”) Alisema Mhe. Waziri.
Mhe. Waziri pia ameahidi kumpatia Kompyuta moja Mkuu wa shule kwa ajili ya matumizi ya kiofisi.
Mwisho Mhe. Waziri alipata fursa ya kuongea na Wanafunzi wote ambapo aliwaasa kusoma kwa bidii huku akiwahimiza zaidi watoto wa kike kwakuwa hawafanyi vizuri katika mitihani ukilinganisha na ufaulu wa wavulana.
Amesema kuwa, Serikali ya awamu ya tano inajitahidi kuangalia maeneo yenye upungufu wa Wataalam mbalimbali ili iweze kutatua changamoto mbalimbali ambapo elimu bora inahitajika katika kuwapata wataalam watakaoweza kutatua mapungufu hayo ndiyo maana inajitahidi kutoa elimu bure kwa sasa na kuendelea kuhimiza wanafunzi kusoma kwa bidii hasa wasichana ili elimu itolewayo iwe sawa kwa wote pasipo ubaguzi na kuweza kumkomboa msichana.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (kulia) akimsikiliza mmoja wa wanafunzi wa Kidato cha Nne wakati wa ziara yake Janda Sekondari Machi 4, 2019.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz