Timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya ya Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe (CHMT) ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo George E Mbilinyi leo tarehe 26 Agosti 2024 imekaa kikao kujadili hatua zilizochukuliwa ili kujikinga na ugonjwa wa Mpox ambao umesharipotiwa katika Nchi za jirani.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji amewaasa watumishi wa idara ya afya kuchukua tahadhari mapema kuhakikisha Nchi inaendelea kuwa salama.Mnamo tarehe 03 Agosti mwaka huu 2024 Wizara ya Afya ilitoa tahadhari kwa umma kuhusu ugonjwa wa Mpox,Katika kipindi chote Wizara imeendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa ugonjwa huu duniani. Aidha tarehe 14 Agosti 2024 Shirika la Afya Duniani lilitangaza ugonjwa wa Mpox kuwa niDharura ya Afya Kimataifa.
#buhigwefahariyetu
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz