Wilaya ya Buhigwe kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) yaadhimisha siku ya Afya na lishe Kijijini katika kijiji cha Bweranka kata ya Buhigwe Wilaya ya Buhigwe kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo utoaji wa Elimu ya lishe kwa Wananchi,Elimu ya kilimo bora kwa Wakulima,namna bora ya kuandaa chakula chenye virutubisho na Utunzaji wa chakula.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina ambaye alikuwa mgeni rasmi .
Akizungumza na Wananchi Kanali Michael Ngayalina amewasihi Wananchi kula chakula kwa kuzingatia maelekezo ambayo yanatolewa na Wataalam mbalimbali wa Afya.
Aidha ameongezea kwa kuwaasa Wananchi kupokea na kuzingatia Elimu inayotolewa na Wataalam mbalimbali wa Afya kwa ajili ya kuwa na familia ya watu wenye Afya Imara.
Sambamba na hilo amewataka kuepuka maradhi kwa kuua wadudu katika maji pamoja na mazingira yanayotuzunguka.
Bi Stella Kimambo ni Afisa Lishe kutoka FAO amewashauri Wananchi hao kutumia vyakula
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz