Klabu ya Michezo ya Wilaya ya Buhigwe Sports Club rasmi imefunguliwa leo tarehe 18 mwezi Januari mwaka 2025 kwa mchezo wa mbio fupi maarufu kama jogging.
Klabu hiyo ikijumuisha michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa Mpira wa Miguu,mpira wa pete,mpira wa wavu,mchezo wa mbio fupi au jogging.
Akizungumza mlezi wa timu hiyo ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina amesema kuwa michezo hiyo ikawe chachu ya maendeleo kwa kufanya kazi kwa bidii pamoja na kujipatia ajira.
Aidha amesisitiza kufanya mazoezi kama ambavyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na mama Samia Suluhu Hassani imekuwa wakisisitiza ili kutunza Afya.
Kwa upande wake Mgeni mualikwa ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu amesema kuwa leo isiwe mwisho wa kushiriki michezo hiyo hivyo watu wote kuweka utaratibu wa kufanya muendelezo wa kufanya michezo hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ambae pia ni mshauri wa klabu hiyo amewashukuru wote walioshiriki mbio hizo na kuwaahidi kuwa huo ni mwanzo na wao kama viongozi wapo tayari kuwasapoti ili klabu hiyo ifike mbali zaidi.
Mchezo huo wa mbio fupi maarufu kama jogging umefanyika kwa kuwakaribisha wageni kutoka Kigoma manispaa wanaojulikana kama Mwisho wa reli jogging Club.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz