Katika Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo Kimkoa yalifanyika Wilayani Buhigwe, Mhe. Thobias Andengenye, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Amezindua Mradi huo wenye Dhamani ya Bilioni Moja na Milioni Mia sita (1,600,000) ambapo amewataka Wananchi kuendelea Kuilinda Miundombinu ya maji
Akihutubia Wananchi kwenye Viwanja vya Buhigwe Centre, RC Andengenye amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuona Kigoma ni sehemu sahihi ya Kuwekeza rasilimali Fedha kwa kuipatia Miradi mabali Mbali ikiwemo hiyo ya Maji, Elimu kama Ujenzi wa Chuo cha Uhasibu na TEHAMA pamoja Afya.
Kwa Mkoa wa Kigoma maadhimisho yalifanyika Wilayani hapo ambapo Aprili 25 yalitanguliwa na Uzinduzi wa Miradi mbali mbali ya Mradi wa Kunusuru Kaya Masikini TASAF kwa Mhe. Kanali Michael Ngayalina alishiriki kupanda Miti zaidi ya elfu sita kwenye maeneo ya Rusaba na Kibwigwa kabla ya Kuzindua Barabara iliyoboreshwa na wanufaika hao
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz