Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe iliandaa mchezo wa uhamasishaji wa uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Shule ya msingi Buhigwe ukizikutanisha timu mbili ambazo ni Buhigwe football Club na Munzeze football Club.
Akizungumza na Wananchi waliohuduria kushuhudia mchezo huo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndugu George Mbilinyi alisema kuwa waliandaa mchezo huo maalumu kwa ajili ya kuhamasisha Wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
“Tuliandaa mchezo huu maalum kwa ajili ya kuhamasisha kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura lakini pia Serikali iliandaa mpango ili kufikia wakati wa uchaguzi kila mwenye sifa ya kupiga kura apate kupiga kura”alisema Mbilinyi.
Aidha aliwaasa kuendelea kujitokeza kwa wingi ili kupata vitambulisho vitakavyowawezesha kushiriki katika uchaguzi
“Kuanzia jana huduma ilishaanza katika vituo mbalimbali kwahyo tunatoa hamasa kwa wanamichezo wote tujitokeze kujiandikisha,Kupiga kura ni haki ya kila mtanzania kwa kila mwenye sifa ya kupiga kura na kitambulisho hicho pia kitakusaidia katika shughuli za kiserikali kama utambulisho wako”ameeleza Mbilinyi.
Naye meneja wa bank ya Nmb tawi la Buhigwe Pendo aliwahimiza Wananchi wote kujihusisha katika michezo sambamba na kuwasihi kujiandikisha katika uboreshaji wa daftari la wapiga kura.
“Niwape motisha vijana wote kujihusisha na michezo lakini ikiwa sambamba na ujumbe ambao tumekuja nao,tujiandikishe katika daftari la wapiga kura,vijana wote ni chachu,ndo viongozi wa sasa,kesho na siku zijazo hivyo hakikisha unajali haki yako ya msingi”amesema Pendo.
Mchezo huo ulimalizika kwa timu ya Munzeze kuibuka kidedea kwa goli moja bila na kupokea zawadi ya fedha taslimu sh 50,000 na mpira wa miguu mpya na mshindi wa pili kupokea fedha taslim sh 100,000 ,zawadi zote zikitolewa na bank ya NMB wilaya ya buhigwe.
MWISHO.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz