Baba Askofu Emmanuel Bwata wa kanisa la Anglican Kasulu leo tarehe 14 April 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George Emmanuel Mbilinyi kufuatia mualiko wa Mkurugenzi kuja kutembelea ofisini kwake.
Kwa pamoja wamezungumza mambo mbalimbali ikiwemo suala la makanisa kuhimiza waumini kushiriki kikamilifu uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu wa 2025 na kuelezea athari kwa Wananchi kutoshiriki uchaguzi mkuu kwa jamii.
Aidha Mkurugenzi amesisitiza kuwa kanisa lina wajibu wa kuhimiza ulinzi na amani katika taifa letu hasa kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Ameongezea kwa kusema kuwa wapo wanasiasa wanalenga kuleta machafuko katika nchi na ni wajibu wa viongozi wadini kukemea jambo hilo na kusisitiza kuendelea kudumisha ushirikiano kati ya Serikali na vyombo vya dini.
Baba Askofu alipata nafasi ya kusalimiana na watumishi na kuwasihi kufanya kazi kwa bidii kwa manufaa ya Nchi pamoja na kumtanguliza Mungu katika kila jambo.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz